0


Mama Mzazi wa Mwanafunzi anaedaiwa kubakwa, Mary Mkombola akisimulia juu ya tukio la ubakaji lililompata Mwanae na kusababisha ujauzito mbele ya waandishi wa habari Kulia ni Martha Danie (17)  anayesoma shule ya City Sekondari kidato cha tatu aliyefanyiwa kitendo hicho.

Mwanasheria Mfawidhi Mkazi wa kituo cha msaada wakisheria cha Tanzania Legal Aid Centre (TALAC), Godwin Ngongi akifafanua jambo kuhusu kitendo cha ubakaji alichofanyiwa Mwanafunzi wa kidato cha tatu Martha

Nabii Elisha Muliri anayetuhumiwa kwa ubakaji


 NABII Elisha Muliri wa kanisa la Ebeneza mjini hapa ameingia matatani baada ya kudaiwa kumbaka na kumtia mimba  mwanafunzi na kukatiza masomo yake huku kutishia kumuua.
Akisimulia tukio hilo mbele ya waandishi wa habari mwanafunzi huyo Martha Daniel [17] kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya City ilyopo manispaa ya Dodoma alisema kabla ya kufanyiwa kitendo hicho alikuwa anaangushwa na mapepo.
Martha alisema baada ya kuhangaika kwa muda mrefu bila mafanikio walipata taarifa za ujio wa nabii huyo mjini humo na wapofika ili kupata msaada wa kuombewa mapepo hayo yalilipuka na binti akaponywa hata leo na kuahidiwa mbele ya kanisa kusaidiwa ada na Nabii huyo.

Binti huyo alisema baada ya kuponywa akaendelea kwenda kusali kanisani hapo ambapo kutokana na kila mtu anayefika na kufanyiwa maombi huacha mawasiliono kwenye vikaratasi, na Juni 8 mwaka huu majira akapigiwa simu na Nabii huyo akipewa maelekezo ya kufika nyuma ya ukumbi wa Paradise ambapo walikuwa wakifanyia ibada.
Anatanabaisha kuwa baada ya kuonana Nabii alimwambia aingie kwenye Gari akaingia akifikili kuna heri akapewa soda aina ya Fanta orange alipokunywa akapoteza fahamu na alipokuja kuzinduka alijikuta akiwa nyumba za kulala wageni makole na Nabii akiwa amemlalia kama alivyozali huku akiangalia mkanda wa Ngono.

‘’Wakati nataka kupiga kelele alinitishia kwamba ataniua kama nitathubutu kumwambia mtu yoyote jambo hilo, akanipiga kofi na kuniambia yeye hawezi kunilipia ada bure kwa sababu mimi siyo ndugu yake lazima lazima alale na mimi mara 5 kwa hiyo bado mara 4 na kunisisitiza asisikie popote kuwa alinifanyia hivyo’’, alisema Mwanafunzi huyo

Kwa upande wake Mama mzazi wa mwanafunzi huyo Mary Mkombora alisema alimpeleka kuombewa kutokana na kusubuliwa na mapepo tangu akiwa Darasa la sita na wakakubaliana na Nabii huyo kumlipia ada kwa awamu hivyo akachukue 50,000 kila mwezi ili kukamilisha 400,000 inayotakiwa shule.

Nilimgundua yupo tofauti kuanzia mwezi wa saba nilipomuuliza alisema yeyue haelewi siku moja nikamshuhudia akitapika asubuhi ndipo nilipochapa na kumfukuza nikapigiwa simu na waliompokea kua mtoto kapewa mimba hiyo na Nabii kwanini nimemfukuza ndipo nikachoka, alipopimwa alikuwa na mimba.

Alisema Nabii huyo ambaye alikuwa Mume wa mwimbaji Marufu wa Nyimbo za Injili marehemu Anjera Chibalonza kwa sasa hajulikani alipo japo mara kadha wasaidizi wa kanisa hilo ambalo limebadilishwa jina kutoka Shakinah Pentecostal Church na kuitwa Ebeneza wamekuwa akitaka Suruhu.

 ‘’sasa hivi mimi na mtoto wangu tumekuwa tukiishi mashakani baada ya Msaidizi wake Nabii Monica  nimpe Martha akamtoe mimba kwa ataaramu anaowajua wao, siku ambayo alichukua kadi yenye namba za simu na kufuta meseji zote mwanangu alizokuwa akiandikiwa na Nabii,’
Nabii huyo kwa sasa hajulikani alipo na hata alipotafutwa kwa simu yake ka mkono 0756 409118 ilikuwa amezimwa na msaidizi wake Nabii Monica Nyambura raia wa nchini Kenya anakotoea Elisha Muliri alisema yeye hawezi kuongelea jambo hilo kwakua yeye ni mgeni ameachiwa kanisa hilo baada ya mwenyeji wake kuwa safarini hivya asubiliwe hatachelewa.

Tukio hilo limefikishwa katika kituo cha sharia cha Tanzania Legal Centre [TALAC] na mwanasheria mfawidhi mkazi Dodoma Godwin Ngongi tayali ameshamuandikia mkuu wa kituo cha polisi kati barua ya kuwataka kumkamata mtuhumiwa huyo ili afikishwe kwenye vyombo vya sharia na pia kuepusha  mwanfunzi huyo na hatari nyingine.

Jeshi hilo limekiri kuwa na taarifa ya tukio hilo na kwamba wanaendelea na  uchunguzi

Post a Comment

AddThis

 
Top