Michael Pius(kushoto) na Hassan Dilunga(kulia).
Kikosi hicho kinajumuisha wachezaji 16 walioitwa katika kikosi cha Taifa Stars kilichotajwa awali na wengine 16 kutoka Future Young Taifa Stars.
Dar es Salaam. Kocha Mkuu wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Kim Poulsen amewajumuisha kwa mara ya kwanza chipukizi watano katika kikosi cha wachezaji 32 kinachojifua kwa ajili ya pambano dhidi timu ya Taifa ya Kenya (Harambee Stars).
Taifa Stars na Harambee Stars zitacheza katika pambano la kimataifa la kirafiki litakalopigwa Novemba 19 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Chipukizi hao ni Ismail Gambo, Faridi Musa, Joseph Kimwaga (Azam), Elias Maguli (Ruvu Shooting) na William Lucian (Simba),
Maguli alionyesha kiwango cha kuvutia katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu uliomalizika hivi karibuni na kupachika mabao tisa na kukamata nafasi ya pili kwa ufungaji nyuma ya Amisi Tambwe wa Simba aliyezamisha mabao 10.
Pia, Kim amewaondoa katika kikosi hicho mshambuliaji wa Azam, John Bocco na beki wa pembeni wa Yanga, David Luhende ambao ni majeruhi.
Kikosi hicho kinajumuisha wachezaji 16 walioitwa katika kikosi cha Taifa Stars kilichotajwa awali na wengine 16 kutoka Future Young Taifa Stars.
Kabla ya kuteua wachezaji 16 wa kuunda Taifa Stars kambi ya Future Taifa Stars iliyoanza Novemba 9 ilikuwa na wachezaji 30.
Kikosi kamili cha Stars kilichotangzwa hivi karibuni na na Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania, Boniface Wambura
ni makipa Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga), Deogratias Munishi (Yanga) na Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya).
Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting), Nadir Haroub (Yanga) na Said Moradi (Azam).
Viungo wakabaji ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa) na Vincent Barnabas anayechezea Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Viungo wachezeshaji ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jonas Mkude (Simba), Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na William Lucian (Simba).
Post a Comment