0


SEKUNDE chache kabla ya mwamuzi Mohamed Theofile wa Morogoro hajamaliza pambano la Ligi Kuu ya Bara kati ya Simba na Kagera Sugar, mashabiki wanaodhaniwa kuwa ni wa Simba, wamevunja viti zaidi ya 100 na kuvirusha uwanjani imefahamika.

Mashabiki hao wanaodhaniwa ni SIMBA wamevunja na kuvirusha uwanjani viti hivyo baada ya mwamuzi huyo kuwapa Kagera penalti iliyofungwa na Salum Kanoni.

Mashabiki hao ambao licha ya kuwa walikaa katika majukwaa tofauti, waliweza kufanya kitendo hicho kwa kile kilichoelezwa baadaye kwamba ni kupingana na maamuzi ya mwamuzi huyo.

Viti vilivyovunjwa vingi vina rangi ya chungwa na bluu ambavyo kwa haraka haraka idadi yake inaweza kuwa zaidi ya 100.

Kutokana na hali hiyo, askari wa Jeshi la Polisi walilazimika kulipua mabomu matatu ya machozi ili kuwatuliza mashabiki hao walioonekana kuwa na hasira.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura ameuambia mtandao huu kwamba, kwa kitendo hicho kamati ya mashindano na ile ya nidhamu zinaweza kukaa na kutathimini uhalibifu uliofanywa na mashabiki hao kisha timu husika kuwajibika kulipa.

“Kila mtu ameona kilichotokea na vurugu za kuvunja viti zilianza tangu wakati wa mapumziko hivyo uchunguzi utafanyika na klabu iliyohusika italipa faini kama utaratibu ulivyo,” alisema Wambura kwa kifupi. 
Kipa wa akiba wa Simba Abel Dhaila akimlalamikia mwamuzi wa akiba baada ya mwamuzi wa kati kutoa penati katiaka dakika za majeruhi.

Kipa wa akiba wa Simba, Abel Dhaila, na Kocha Mkuu, Abdallah Kibaden, wakimlalamikia mwamuzi wa akiba baada ya mwamuzi wa kati kutoa penati katika dakika za majeruhi.
 Wachezaji wa akiba wa Simba wakisikitika baada ya kuamuliwa kupigwa penati hiyo
Askari wakimkamata shabiki aliyekutwa baada ya mashabiki y amasahbiki hao kuvunja viti na kuanza juruka uwanjani.
 Askari wakiendelea kudhibiti vurugu

Sehemu ya viti iliyoharibiwa 


Patashika langoni mwa Kagera Sugar.
Kiungo wa Kagera Sugar, George Kavila (kulia) akimtoka mshambuliaji wa SImba, Amis Tambwe, wakati wa mchezo huo.

Amisi Tambwe akidhibitiwa

Ramadhan Singano wa Simba (kushoto) akijaribu kumtoka beki wa Kagera Sugar, Malegesi Mwangwa
Hatari tena langoni mwa kagera


PENALTI iliyopigwa dakika za nyongeza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Bara uliozikutanisha Simba na Kagera Sugar muda mfupi uliopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ilibadili matokeo na kufanya mchezo huo kuisha kwa sare ya bao 1-1.
 
Huku mashabiki wengi wakidhani mechi hiyo ingemalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0, mwamuzi Mohamed Theofile wa Morogoro aliipa penalti Kagera wakati mwamuzi wa akiba akiwa ameshaonyesha dakika nne za nyongeza na mashabiki kutoamini kilichotokea.

Beki Joseph Owino ndiye aliyesababisha penalti hiyo baada ya kumchezea vibaya Daudi Jumanne wa Kagera ndani ya eneo la hatari ambapo, beki Salum Kanoni wa Kagera alifunga penalti hiyo na sekunde chache baadaye mwamuzi alimaliza pambano hilo.

Awali Simba ilipata bao la kuongoza dakika ya 45 lililofungwa na Amisi Tambwe baada ya mabeki wa Kagera kujichanganya katika kuokoa. Bao hilo lilidumu hadi timu hizo zilipoenda kupumzika.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi lakini hadi dakika ya 85, hakuna timu iliyoweza kupata bao kutokana na safu zote za ushambuliaji kutokuwa makini.

Mshambuliaji wa Kagera, Themi Felix pamoja na winga Paul Ngwai leo hawakuweza kufurukuta mbele ya mabeki wa Simba waliokuwa wakiongozwa na nahodha wao Nassor Masoud ‘Chollo’.

Nao washambuliaji wa Simba, Tambwe na Betram Mombeki hawakuweza kufurukuta kutokana na mabeki wa Kagera kucheza kwa nguvu zaidi wakiongozwa na Maregesi Mwangwa ambaye ni nahodha wao.

Muda mfupi baada ya Kanoni kufunga bao, alienda kushangilia akiwa sambamba na wenzake mahala ambapo mashabiki wa Simba wamekaa na kuzua tafrani ya kurushiwa chupa za maji na viti vilivyovunjwa na mashabiki hao.

Kutokana na hali hiyo, askari wa Jeshi la Polisi waliokuwepo uwanjani hapo walilazimika kulipua mabomu matatu ya machozi ili kutawanya mashabiki hao, hali iliyozua hali ya taharuki uwanjani hapo.

Matokeo haya yanaifanya Simba kufikisha pointi 21 na kubaki katika nafasi ya nne baada ya kucheza mechi 12.
Nayo Kagera imepanda hadi nafasi ya tano ikiwa na pointi 17.

LIVE SCORE/ SIMBA SC 1-KAGERA SUGAR 1
 


Mashabiki wa Simba wanang'oa viti vya uwanja wa taifa na mashabiki wanapambana na Polisi ambao wanalipua mabomu ya machozi. 

Dk 90+5 FULL TIME! Simba 1-1 Kagera. 

Dk 90+4 GOOOOO....! Salum Kanoni anaipatia Kagera bao la kusawazisha kwa njia ya penalti. Simba 1-1 Kagera. 

Dk 84 Tambwe anachezewa faulo na Martin Muganyizi. Simba 1-0 Kagera. 

Dk 73 Kagera wanapiga faulo na kukosa. 

Dk 73 Kipa wa Simba anachelewesha mpira na mwamuzi anaamuru faulo ipigwe kuelekea lango la Simba. Simba 1-0 Kagera. 

DK 60 Simba 1 - 0 Kagera 

Dk 57 Timu zinashambuliana kwa zamu na Kagera wanaonekana wameamka. 
Kipindi cha pili kinaanza

Dk 45 HALF TIME...! Simba 1-0 Kagera. 

Dk 45 GOOOOO...!  Simba imepata bao la kwanza kupitia kwa Amisi Tambwe ambae aliwatoka mabeki wa Kagera, Salum Kanoni na Ernest Mwalupani. 

DK 40 Simba wanalisakama lango la Kagera wakisaka goli. Ila milango bado ni migumu.

DK 30' Simba 0-0 Kagera Sugar 

Dk 21 Kagera wamefanya mabadiliko ya kipa, katoka agaton anthony ambaye ameumia bada ya kugongana na Tambwe kaingia hannington kalyesubula. 

DK 10 - Simba 0-0 Kagera Sugar

DK 5 Timu zinacheza soka taratibu kwa kusomana

Dk 00 MPIRA UMEANZA! 

Simba: Abuu Hashimu, Nassoro Masoud 'Chollo', Issa Rashid, Joseph Owino, Hassan Khatib, Jonas Mkude, Ramadhani Singano, Said Ndemla, Betram Mwombeki, Amisi Tambwe na William Lucian

Kagera Sugar: Agaton Antony, Salum Kanoni, Martin Muganyizi, Ernest Mwalupani, Malegezi Mwangwa, Zuberi Dabi, Benjamin Asukule, George Kavilla, Themi Felix, Daudi Jumanne na Paul Ngwai








Post a Comment

AddThis

 
Top