EXCLUSIVE...WABUNGE WAFANYA FUJO BUNGENI KABLA YA SAA SABA MCHANA WA LEO
Ndani ya bunge mchana wa leo kabla ya saa saba mchana ndivyo hali ilivyokuwa
Wakati kikao cha bunge kikiendelea kujadili muswada wa mabadiliko ya sheria ya katiba ikaonekana mheshimiwa Tundu lissu wa Chadema ambaye alipewa nafasi ya kuchangia kwa mujibu wa taratibu za kibunge akasema kuwa muswada huo usiendelee kujadiliwa kwani una mapungufu
Akitoa sababu za kutaka kusitishwa kujadiliwa muswada huo mheshimiwa Lissu amesema kuwa wajumbe waliyochaguliwa kwenda kujadili muswada huo si watu makini
Naibu Spika wa bunge mheshimiwa Job Ndugai akamuamuru mheshimiwa Tundu lissu akae chini kwa mujibu wa taratibu za kiti chake kama Naibu Spika wa bunge la jamunhuri ya muungano wa Tanzania
Wakati muswada ukiendelea kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani bungeni mheshimiwa Freeman Mbowe aliomba muongozo kuhusu muswada huo lakini Naibu Spika alimwambia akae chini ndipo Mbowe akagoma kukaa chini
Baada ya kugoma kukaa chini Naibu spika akaita askari wamtoe nje ndipo ilipotokea kutoelewana na kusababisha mzozo uliyopelekea kusimama kwa shughuli za bunge kwa dakika kadhaa
Lakini baadae walinda usalama wa bungeni waliyoamriwa na Mheshimiwa Ndugai walifanikiwa kumtoa nje ya Bunge Mheshimiwa Freeman Mbowe na Naibu akaomba radhi na kikao cha bunge kikandelea kama kawaida
Post a Comment