0



Ni mtu wa karibu sana kwa Muziki wa Kongo na shabiki namba moja wa JB Mpiana akisifika kwa utunzaji wake ambapo kwa kuthamini hilo JB Mpiana ameshamtungia nyimbo kadhaa mbali na kumtaJa kwenye karibu kila wimbo wake.




Ni mfanyabiashara wa madini na mtoto wa mjini mtafuta maisha ambaye anatumia kila njia kujipatia kipato chake. Harusi hii mbali na kutumbuizwa na bendi kadhaa ilihudhuriwa na matajiri na watu maarufu wakiwemo wanamuziki mbalimbali wa Congo.

Kwa mujibu wa mtangazaji maarufu wa Luninga na mtengenezaji wa vipindi vya majadiliano almaarufu kama Zacharia Bababaswe anasema kwamba Harusi hii pia imetajwa kuingia kwenye historia ya moja ya harusi kubwa kupata kutokea kwa Mkongoman si tu ukubwa wa Harusi bali iliyogharimu pesa nyingi sana.

Zadio amemuoa mpenzi wake wa siku nyingi binti mrembo anayejulikana kwa jina la Carole katika sherehe zilizofanyika huko huko Ufaransa. Zadio au ZK kama alivyoitwa na mashabiki wake anajulikana kwa style yake ya utunzaji awapo jukwaani ambapo kuna wakati anatunza mpaka dola zaidi ya 20,000 katika show moja.



Post a Comment

AddThis

 
Top