Majonzi! Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’, Ali Choki amepata pigo kubwa la kufiwa na mkewe, Shuea Hamis ‘Mama Shuu’ baada ya kuugua kwa muda mrefu.aliyekuwa mke wa ally choki marehemu shuea hamis mama shuu enzi za uhai wake
Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa masikitiko, Choki alisema kwamba mke wake ameugua kwa muda wa miezi tisa akisumbuliwa na tatizo la mguu.
Alisema kwamba katika jitihada za matibabu, mkewe huyo alitibiwa nchini India ikashindikana, akarudishwa nyumbani mpaka mauti yalipomfika usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita.
“Kweli alikuwa akipata mateso makubwa kwani alikuwa hatembei analala tu ndani hivyo kutoa nafasi kwa magonjwa mengine kumshambulia.
“Ukweli nimeumia kwani alikuwa ni mshauri wangu mkuu na ndiye alikuwa kila kitu kwangu.
“Alikuwa akinisapoti sana kwenye kazi yangu ya muziki lakini ndiyo hivyo Mungu amempenda zaidi sina la kufanya,” alisema Choki kwa majonzi.
“Alikuwa akinisapoti sana kwenye kazi yangu ya muziki lakini ndiyo hivyo Mungu amempenda zaidi sina la kufanya,” alisema Choki kwa majonzi.
Ali Choki akiwa kwenye picha ya pamoja na mkewe enzi za uhai wake.
Choki alisema mipango ya mazishi ilifanyika nyumbani kwake Tuangoma, Kigamboni jijini Dar na mazishi ya mkewe yalitarajiwa kufanyika jana Jumapili, saa 10:00 jioni katika Makaburi ya Maduka-Mawili, Chang’ombe, Dar.Mama Shuu alikuwa mdau mkubwa wa muziki wa dansi Bongo hivyo ni pigo kubwa kwa tasnia hiyo. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.
Post a Comment