0
Habari zilizo tufikia punde,ambazo bado zahitaji kusibitishwa, zaashiria kwamba Msanii Supersatar wa CONGO WERRASON NGIAMA MAKANDA LE ROI DE LA FORET yuko chini ya ulinzi wa polisi Inchini Ufaransa ( FRANCE )Habari tulizo waletea majuzi kwamba Msanii huyo yuko Jijini Paris, kumalizia kazi ya Album inayosubiriwa na wengi ” FLECHE INGETA “. Katika dhiara yake hiyo, WERRASON kawakivutio kwa Watu wengi,hasa kwa wale wapenzi wake na Wapenda Muziki wa Rumba kwa jumla. Kwenye mahojiano yake na Vyombo vya habari Jijini Paris, WERRASON kawaomba kwa wote wale wanao hitaji MAJINA yao yatajwe ( LIBANGA ) kwenye Album FLECHE INGETA, basi awasiliane na Mpambe wake Namba Moja SANKARA DE KUNTA. kupitia na hii 0033751261721

Kutokana na wito huo, basi Mamia ya Watu walijitokeza ili kufaanikisha na kuhakikisha wanatajwa Namsanii huyo anaevutia Watu wengi popote aendako,Ushahidi ni kwamba Tokea alipo wasili  JIJINI PARIS, kaacha gumzo kutokana na Umati wa Watu unaomzingira popote apitapo. Hadi Baadhi ya Watu wakawa wanajiuliza hao wa COMBATTANTS WAKO WAPI ?

Akiwa kwenye STUDIO kuendelea na kazi ya Album yake, huku akiwa PIA anatoza Pesa za Watu wapenda LIBANGA, yasemekana kina cha chini ilimtu atajwe ni EUROS 150, Mashahidi wanasema  kachukua pesa papo hapo ya Watu zaidi ya  50.waliojipendekeza kwa zoezi hilo.
Maskini kwake ,hajatarajia kabisa yaliyomkuta, Kumbe kati ya Watu hao walikuwepo pia wabaya wake, waliomgea PESA FEKI ZA EUROS.

Akiwa  MADUKANI KWENYE MTAA MAARUFU JIJINI PARIS WA CHAMPS – ELYSÉES, baada ya kufanya Shopping, Mmoja wa WAFANYABIASHARA kagundua katapeliwa na pesa Feki, ndipo kawataarifu polisi, nao bila kusita wakaenda kumsubiria LE PHÉNOMÈNE WERRASON NGIAMA MAKANDA Hotelini kwake. Hadi Wakati huu Bado hajaachiliwa na Polisi chaeleza chanzo chetu.

Kutokana na Mkasa huo, WERRASON atashindwa kabisa kusafiri Inchini AMERICA anakosubiriwa kwaajili ya kupewa Tuzo lake la GENERIC BORA AFRICA KUTOKANA NA ALBUM ” TECHNO MALEWA “.
SWALI : NINANI YULE KAMTENDEA UNYAMA WERRASON, NI WA COMBATTANTS ? au WAPENZI NA MASHABIKI WA KOFFI OLOMIDE ? historia itatupatia Sheria.

Post a Comment

AddThis

 
Top