0

Mgeni rasmi katika mapambano mawili ya ngumi
ya kimataifa ,mkuu wa wilaya ya Hai ,Novatus Makunga akiteta jambo na
Mwenyekiti wa chama cha Ngumi mkoa wa Kilimanjaro Elikunda Kipoko
wakati wa mapambano hayo  


Mapambano ya utangulizi yakaanza

Mgeni rasmi katika mapambano mawili ya ngumi
ya kimataifa ,mkuu wa wilaya ya Hai ,Novatus Makunga akizungumza
wakati wa mapambano hayo kati ya Bondia Said Yazidu(Tanzania) na
Djamel Dahou(Aljeria) 

Muandaaji wa Pambano hilo,Andrew George
akionesha mkanda wa Ubingwa wa Afrika ulikuwa ukigombewa na Bondia
Alibaba Ramadhan(Tanzania) na Aleck Mwenda(Malawi) 
Mgeni rasmi ,Novatus Makunga akonesha mkanda
huo kwa mashabiki. 
Pambano likaanza kati ya
Bondia,Alibaba(Mwenye Bukta nyekundu) na Aleck Mwenda(Mwenye Bukta
nyeusi) 
Alibaba akajaribu kupiga ngumi kadri
alivyoweza

Alibaba akaenda chini mara kadhaa lakini
alinyanyuka


Round 10 zikamalizika uamuzi wa majaji
ukingojewa. huku dalili zikionesha dhahiri ,Aleck Mwenda atakuwa
ameshinda
 
Akiwa amebebwa na wamalawi wenzake na
kushangilia ,hakuamini alichosikia masikioni mwake baada ya mshindi
kutangazwa Alibaba.
Furaha ikahamia kwa
Alibaba.
Mashabiki wakaingia ulingoni kwa Bondia na
Chupa za Bia

Kamanda wa Polisi wa wilaya OCD, Deodatus
Kasindo akamkabidhi mkanda Alibaba
Alibaba akifurahia mkanda wake wa Kwanza
baada ya kutangazwa Bingwa wa  Ngumi
Afrika.  




Furaha ya Ushindi.
 


Likafuatia Pambano la Ubingwa wa Dunia Kati
ya Bondia ,Djamel Dahou(Aljeria) na Said Yazidu
 
Mpambano ukaanza.
.
Kila mmoja akamvizia
mwenzake.


Bondia Yazidu akapigwa vitasa
kadhaa
 
Akakaaa kwa mara ya kwanza  
Akasimama kisha akajitutumua ,akapigwa
kitasa tena , - See more at: http://shaffihdauda.com/?p=6392#sthash.41f71TBR.dpuf
.
Akasimama kisha akajitutumua ,akapigwa
kitasa tena 

Akakaa kwa mara nyingine


. Akasimama tena akachezea ngumi za kutosha

 
Zikampeleka chini kwa mara ya
tatu
. Akanyanyuka kwa Mbinde
 


  Ikashindikana na Bondia ,Dahou akashinda kwa
KO ndani ya dakika 2 na sekunde 7 katika round ya
kwanza

Dahou akatangazwa Bingwa.
 





Post a Comment

AddThis

 
Top